Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, amepigwa risasi na polisi baada ya kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.
Kibet wenye umri wa miaka 25, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na polisi waliokuwa wakifanya doria katika eneo hilo hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.
Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena-Mararo tukio hilo litokea Jumatatu na mtuhumiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa ajili ya matibabu.
Siku moja kabla ya tukio hilo kutokea Kibet aliandika katika mtandao wake wa Facebook kuwa atavamia Ikulu.
Ikulu ya Nairobi Kenya
Tukio hilo limezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini humo huku baadhi watu wakiamini huenda mwanafunzi huyo alichukua hatua hiyo baada ya kutumia kilevi chochote kwasababu mtu aliye na akili timamu hawezi kufanya hivyo.
Kwa sasa Kibet anaendelea na matibabu katika katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta nchini humo.