Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewaasa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuendelea kuwa na ujasiri, umoja na mshikamano katika kulinda na kutetea maslai ya chama na Taifa.

Akizungumza na mamia ya Vijana wa CCM katika uzinduzi wa kampeni ya "Nyamagana ya Kijani" Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amesema Vijana wa CCM waendelee kuwa na ujasiri, umoja na mshikamano katika kulinda na kutetea maslahi ya Chama na Taifa.

Akifafanua suala hili Ndugu Polepole amesema Vijana wa CCM ni ngao ya Viongozi wa CCM, waendelee kumlinda, kumtetea na Kumuunga Mkono Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania na kuwapinga viongozi wanaotaka kumuangusha kwa hila na wasiofuata utaratibu kupitia vikao.

"Ni waombe sana chukueni mazuri ya Viongozi wetu na yale mabaya nendeni kwenye vikao mkawapinge, msikubali waharibu kazi nzuri ya Ndg. Magufuli inayojenga mustakabali wa leo na kesho yenu" amesisitiza Ndugu Polepole

Uzinduzi wa kampeni ya Nyamagana ya Kijani umehudhuriwa na Viongozi wa Chama na Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa wa Mwanza.