Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),  Humphrey Polepole, amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu badala yake wawe suluhisho kwa kufuata malengo ya chama ambayo ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.

Ameyasema hayo jana katika semina ya kuwafunda makatibu wa uenzi wa ngazi zote mkoani humo ambapo amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora ya kutumikia wananchi na kuwasikiliza ili kujua shida zao.

“Hii ni CCM mpya chini ya mwenyekiti Rais John Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani kuna siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni Watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali ”amesema.

Amesema kuwa kwasasa mlango uko wazi na kwamba endapo kuna mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya chama hicho chini ya Rais Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi.