Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na England Peter Crouch June 3 2019 yeye pamoja na mke wake Abbey Clancy walibahatika kupata mtoto wao wa kiume, hivyo alipoamua kuweka hadharani taarifa hizo Crouch aliandika jina ambalo wengi walijua ndio litakuwa jina la mtoto huyo.

Crouch mwenye umri wa miaka 38 wakati wa utoaji wa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika “Mtoto wetu mzuri wa kiume amezaliwa Jumatatu ya June 3, mama na mtoto Divock Samrat Crouch wanaendelea poa” baada ya maswali kuwa mengi na kuhisi kuwa amemuita mwanae jina la Divock kwa sababu ni jina la kwanza la Origi wa Liverpool aliyefunga goli la pili la Liverpool katika mchezo wa fainali ya UEFA Champions League.

Baada ya taarifa hizo kuanza kuaminika huku wengi wakiamini kuwa Crouch kamuita mwanae jina la pili la Samrat kwa sababu ya mgaha wa kihindi anaopenda kula, ameweka wazi kuwa ile ulikuwa ni utani tu yeye na mpenzi wake bado hawajaamua jina “Mtoto wetu mzuri jina lake bado halijathibitika rasmi litakuwa lipi, kwa bahati mbaya Abs hajapenda jina la Divock Samrat”