Baada ya msanii wa muziki nchini Marekani, Justin Bieber kuomba pambano la ngumi dhidi ya  Muigizaji Tom Cruise, Hatimaye Rais wa UFC, Dana White amepigilia msumari pambano hilo kwa kusema kusema kuwa litakuwa pambano la karne na la kipekee.


Dana White kwenye mahojiano yake na Mtandao wa TMZ, amesema kuwa yeye yupo tayari kutoa refa, wasimamizi na ukumbi kwaajili ya pambano hilo.

“Nimepata simu nyingi kutoka kwa watu wakiniuliza kuhusu pambano hilo, Lakini nakosa cha kuwajibu kwani sijapata taarifa rasmi kutoka kwa wahusika. Nimeona tu mtandaoni kama nyie mlivyoona Bieber ka-tweet akiomba pambano,”amesema White na kuendelea.

“Unajua linapotokea pambano kwa watu maarufu kama wanamichezo, Waigizaji na wanamuziki kila mtu anataka kuona na linakuwa na mvuto sana. Hivyo mimi nipo tayari kwa pambano hilo kama Rais wa UFC nitatoa uwanja, wasimamizi na vitu vingine muhimu. Kwa kweli natamani TOM akubali hata kesho pambano hilo lifanyike,“.

Wiki mbili zilizopita Justin Bieber kupitia ukurasa wake wa Twitter aliomba pambano dhidi ya Tom Cruise huku akishindwa kueleza sababu ya pambano hilo.


Justin Bieber

@justinbieber
 I wanna challenge Tom Cruise to fight in the octagon. Tom if you dont take this fight your scared and you will never live it down. Who is willing to put on the fight? @danawhite ?

225K
3:34 AM - Jun 10, 2019
Twitter Ads info and privacy
84.9K people are talking about this
Kwa upande mwingine, Mkali wa MMA, Conor McGregory amesema yeye yupo tayari Kampuni yake ya McGregor Sports and Entertainment kusimamia pambano hilo.

“Kama kweli Tom Cruise ni mwanaume na atakubali kupambana na Beiber, Kampuni yangu itasimamia mpambano huo. Swali ni Je, Tom una uwezo huo? wakutuonesha kama unavyocheza kwenye filamu zako,“ameandika McGregory.

Mpaka sasa Tom Cruise (54) hajajibu kama yupo tayari kupambana na Justin Beiber (25).

Pambano hilo limeonekana kuvutia mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimshinikiza Tom Cruise akubali mtanange huo.