Mwimbaji wa Bongofleva Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz amesema watumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Instagram ni kama nchi huru inayojiutegemea na sheria zake.

Akiongea kwenye Friday Night Live jana Ijumaa Juni 28, 2019, amesema kitendo cha yeye kupata mtoto kilipokelewa kwa utofauti baada ya watu mbalimbali mitandaoni kuhoji aliwezaje kumpa mtu ujauzito wakati alikuwa mgonjwa.

''Unajua watanzania wa Instagram ni kama wana nchi yao yenye sheria zake na wanaweza kukuhoji kwa kila kitu unachofanya wakitaka tu kujua ukweli wa mambo lakini mtoto yupo na atakuja Tanzania'', amesema.

Ommy ameweka wazi kuwa hivi karibuni mtoto wake atamleta Tanzania muda wowote anasubiri tu hali ya hewa ikae vizuri huku akitania kuwa, ''Ngija Dengue iishe ndio nimlete''.

Pia Ommy alimtambulisha msanii kutoka Kenya aitwaye Petra, ambaye wameshirikiana kwenye ngoma inayoitwa One & Only.