Serikali imependekeza kupandisha kwa ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za nywele bandia zinazozalishwa nchini na asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchi.


Pendekezo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Waziri Mpango ameeleza kuwa "napendekeza kutoza ushuru wa asilimia 10 kwenye bidhaa za nywele za bandia, zinazotengenezwa ndani ya nchi na asilimia 25 zazoagizwa kutoka nje ya nchi lengo ni kuongeza mapato ya Serikali."

Mara baada ya Waziri Mpango kuwasilisha pendekezo hilo kwenye bajeti ya Serikali, ukumbi wa Bunge uliripuka kwa kelele kwa Wabunge wakipiga meza zao wakionesha kufurahia pendekezo hilo.

Aidha katika bajeti Waziri mpando alipendekeza kupandishwa tozo leseni ya magari ya pamoja na kuongez amwaka kutoka miaka 3 hadi miaka 5, kwa mwaka 2018/2019