Msanii anayekuja kwa nguvu katika tasnia ya Bongo Fleva, mwanadada Hamisa Mobetto amesema hakufurahishwa na lawama alizotupiwa na msanii Foby kuwa alikataa kufanya naye kolabl

Hamisa amesema hayo kupitia eNewz ya EATV, ambapo amejitetea kuwa alikuwa nje ya nchi ndiyo maana ilikuwa ngumu kwake kufanya kolabo hiyo.

"Nilikuwa nje ya nchi wakati huo na alikuwa ananipigia simu akaniambia kuna nyimbo anataka tufanye nikamwambia nitumie nyimbo. Mimi nilishajiwekea kuwa kila anayeniandikia nyimbo kama ni msanii lazima nitafanya naye kolabo", amesema Hamisa.

"Sasa sielewi kitu gani kilimfanya afikirie kuwa nimekataa kufanya naye nyimbo. Sikuwahi kumpigia kumuuliza toka hapo kwa sababu nilikereka sana, ni bora angenipigia na kuniuliza kama nili'download' wimbo", ameongeza.

Hivi sasa Hamisa anatamba na wimbo wa 'Boss' alioufanya na Christian Bella.