Baada ya Real Madrid kukamilisha dili la Eden Hazard kutoka Chelsea kwa dau la Euro milioni 150, Hazard amesema amefanya maamuzi magumu kwenye sekta ya michezo.

Hazard amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Madrid ya Zinedine Zidane na anatarajiwa kufanyiwa vipimo Juni 13.

Nyota huyo ametupia jumla ya mabao 110 kwenye michezo 352 baada ya kujiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2012 na alicheka na nyavu mara mbili kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita mbele ya Arsenal.

"Kuondoka Chelsea ni jambo kubwa na gumu ambalo nimelifanya kwangu mimi hasa kwenye suala zima la kitu ninachokipenda ambacho ni michezo na kila muda ni lazima ufanye jambo litakalokuza ndoto yako iwe kweli.

"Sasa ipo wazi na inajulikana kwamba naondoka Chelsea ila naweka wazi kwamba nilikuwa na kipindi kizuri nilipokuwa ndani ya Chelsea na hii sio mara ya kwanza kwa sasa ipo wazi naondoka kupata changamoto mpya," amesema.