Naomba Watanzania wasinitoe akili - Baba Diamond
Baba Mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma amewaomba Watanzania kutomtoa akili kwasababu anaimba muziki kwa sababu kuimba ni kipaji.

Baba Diamond amesema kuwa yeye hana utu uzima kiivyo huku akisema kuwa kuna wazee ambao walikuwepo kwenye mziki na wamekufa wakiimba.

"Naomba Watanzania wasinitoe akili mziki ni kipaji , mimi sina utu uzima ule wa kupita kiwango wa kusemna kwamba too much nadhani ni kawaida na kuna wakubwa wanaoimba zaidi ya mimi wakubwa mpaka wamezeekea na kufa kwenye muziki,"  amesisitiza Baba Diamond.

"Kwahiyo ni vitu vya kawaida atakae taka kunipa sapoti atanipa atakaeona sifai ataachana na mimi wanamuziki wako wengi tu ila tusitoleane ,amemo ya kashfa tukatukanana kwa kitu ambacho leo kipo kesho hakipo."