Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Faustina Mfinanga 'Nandy' amemzawadia gari mpiga picha wake anayefahamika kwa jina la Alley katika siku yake ya kuzaliwa.

Mwanadada huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost video ikionesha walivyomfanyia 'sapraiz' mpiga picha wake na kudai kuwa amefanya hayo kutokana na nidhamu aliyomuonesha tangu wafahamiane.

"Alley nimeishi naye vizuri kwa miaka minne sasa tangu ananipiga picha bure sikuwa na pesa ya kumlipa hadi sasa nimeweza kumlipa, amenifanyia vingi sana sina cha kumlipa namuombea tu azidi kubarikiwa na afanye kazi kwa bidii", amesema Nandy.

Nandy anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake alioshirikishwa na msanii kutoka nchini Kenya, Willy Paul Msafi uitwao Halleluya.