Mzee wa miaka 70 amekamatwa nchini Uganda kwa tuhuma za kulipiga mawe gari ya Rais Museveni likiwa kwenye msafara mwaka jana.

Mzee Omar Risasi Amabua alikamatwa katika Mji wa Arua na baadaye kuhamishiwa katika mahabusu iliyoko Gulu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nile Magharibi, Christopher Barugahare mtuhumiwa huyo atashtakiwa kwa uhaini.

"Tumemkamata kwa sababu amehusishwa na tukio la mwaka jana ambapo gari la rais lilishambuliwa kwa mawe," Bw. Barugahare alisema.

Gari hilo lilishambuliwa Augosti 13, 2018, siku ya mwisho wa kapeini za uchaguzi mdogo wa Manispaa ya Arua.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia mauaji ya kinyama ya Mbunge Ibrahim Abiriga na mlizi wake ambaye alitajuw akuwa ndugu yake.

Tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza vitengo vya usalama kuwatafuta wauaji wa kiongozi huyo .

Abiriga ambaye masomo yake yalitiliwa shaka na wapinzani wake alikuwa mgombea wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM)

Wakimbizi wapenzi wa jinsia moja warudishwa Kakuma
Kampeini ya kumuondoa kitini ilikumbwa na ghasia siku ya mwisho baada ya mwana chama wa Forum for Democratic Change, Kassiano Wadri, kuamua kuwania kiti hicho kama mgombea huru kuonesha dalili ya kushinda uchaguzi huo. Wadri alishinda uchaguzi kama ilivyobashiriwa.

Rais Museveni alikuwa mjini Arua, siku ya mwisho ya kampaini ya uchaguzi mdogo, kumpigia debe mgombea wa NRM Nusura Tiperu, ambaye alishindwa katika uchaguzi huo na hata rufaa aliyowasilisha mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo kutupiliwa mbali.