Mahakama ya wilaya ya Misungwi jijini Mwanza imemuhukumu baba mmoja kwenda jela kutokana na kukutwa na hatia ya kumzalisha mtoto wake wa kumzaa.Mzazi huyo, Jacob Shabani (30) mkazi wa Kijiji cha Wanzamiso, Misungwi alihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanaye wa kuzaa akiwa na umri wa miaka 14.

Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo mtoto huyo alisema “Baba alinipa ujauzito mara tatu, nilizaa mara mbili mtoto mkubwa alifariki mwaka jana kesi ilipokuwa imeanza, mimba moja iliharibika baada ya kunipiga sana, na sasa nina mtoto mdogo ana mwaka mmoja.”.

Mtoto huyo amesema hali hiyo ilitokea baada ya baba yake kutengana na mama yake kuondoka nyumbani wakati yeye akiwa na miaka 12 mwaka 2015 na ndipo baba yake aliza kufanya naye mapenzi.

Kwa upande mwingine, mzazi huyo ameiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu hiyo akidai kuwa yeye ni mzazi na anafamilia inamtegemea