Miaka miwili baada ya kifo chake nchni Ubelgiji, mazishi ya kitaifa yamefanyika kwa kiongozi wa zamani wa upinzani nchini DR Congo Etienne Tshisekedi.

Mwili wake ulisafirishwa nyumbani siku ya Alhamisi kufuatia mgogoro kati ya familia yake na serikali ya iliopita .

Mgogoro huo ulikwisha baada ya mwanawe kuwa rais mwaka uliopita.

Makumi ya maelfu ya watu walihudhuria Ibada ya wafu katika uwanja wa mashahidi mjini Kinshasa wakiongozwa na Askofu Fridolin Ambongo.

Kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo liliwataka wafuasi wake kuhudhuri kwa wingi katika mazishi hayo.

Siku ya Ijumaa , rais wa Rwanda na Angola walikua miongoni mwa idadi kubwa ya watu waliojitokeza ili kutoa heshima yao ya mwisho kwa marehemu kufuatia miaka kadhaa ya uhasama kati ya taifa lake na DR Congo.