Mbunge wa Iramba Magharibi Dr. Mwigulu Nchemba amependekeza kuwa mtindo wa mavazi ambao yeye amekuwa akiuvaa mara kwa mara utumike kama vazi la taifa kwa kile alichokieleza umekuwa ukiwatambulisha watanzania hasa wanapokuwa nje ya nchi.


Dr. Mwigulu ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo juu ya vazi rasmi la taifa.

Mwigului Nchemba ameuliza kuwa "watanzania wakienda nje ya nchi wanatumia skafu, tai bendera ya taifa yani Mwigulu style na wanatambuliwa ni Watanzania, kwanini Serikali isiseme hili ndilo vazi la taifa?.

Akijibu swali hiyo, Naibu Waziri Juliana Shonza amesema kwa sasa mchakato wa kulipata vazi la taifa ulishaanza upya hivyo watahakikisha wanapokea maoni ya watu mbalimbali.

"Kwa sababu mchakato umeshaanza, nimwambie tu maoni ambayo ameyatoa tunayachukua na tutayafanyia kazi", amesema shonza.