Mwanamke aliyefanya tukio la aina yake Mkoani Geita, anayejulikana kwa jina la Happines Shadrack (36), aliyemchinja mwanaye kisha kumkatakata vipande na kumpika supu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.


Kamanda wa polisi  Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi  Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, ambapo amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kubaini kama kosa hilo alitenda kwa kukusudia, na atafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji.

''Bado tunamshikilia ili kubaini mambo mbalimbali na uchunguzi utakapokamilika tutampeleka mahakamani, na kesi yake inahusu mauaji na unajua kesi hizi huwa hazipelekwi katika Mahakama za kawaida huwa zinapelekwa Mahakama kuu''. - Ameeleza.

Tukio hilo lilitokea  Juni 23 mwaka huu, katika kijiji cha Bulige kata ya  Senga Mkoani Geita, ambapo alimpika supu mwanaye wa kumzaa Martha Yakobo (1).