Hatimaye Mtandao wa 5G umeanza kupatikana katika baadhi ya majiji nchini Marekani.

Kampuni ya Verizon imefunga miundombinu ya 5G katika majiji matano ambayo ni; Houston, Indianapolis, Los Angeles, Sacramento na California.

Imeelezwa kuwa, ili kupata 5G lazima uwe kwenye moja ya majiji hayo na uwe na kifaa chenye uwezo wa kunasa na kutumia 5G.