Msanii wa muziki nchini Marekani ambaye pia ni Dj, Thomas Wesley Pentz Jr. maarufu kama Diplo, amefunguka hisia zake juu ya msanii wa muziki wa bongo fleva, Vanessa Mdee.


Kwenye posti aliyoiweka Vanessa kwenye ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo kutoka majuu akaona isiwe tabu na kuja ku-coment chini yake akielezea ni kwa namna gani anavyohisi moyoni mwake, ambapo Vanessa alijibu bila kusita.Inasemekana kuwa Vanessa Mdee ameachana na mpenzi wake wa muda mrefu Juma Jux, na huenda siku za hivi karibuni akampata shemeji mpya kutoka majuu.

Diplo ni kiongozi wa kundi la muziki la Major Lazer la nchini Marekani, ambalo limeshatoa hitsongs kibao kama Lean on ambayo imetazamwa mara bilioni 2.5 kwenye mtandao wa YouTube.