Serikali nchini Ethiopia imethibitisha kuwa Mkuu wa Majeshi nchini humo, Gen Seare Mekonnen ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake akiwa nyumbani kwake.

Gen Seare Mekonnen (TV screen grab)
Gen Seare Mekonnen
Akihutubia taifa kwa njia ya runinga mapema leo asubuhi, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema kuwa tukio hilo limetokea jana jioni mjini Ahmara.

Mwingine aliyeuawa kwenye tukio hilo ni mfanyakazi wa ndani wa Mkuu huyo wa majeshi ambaye alikuwa anamzuia asipigwe na risasi.

Waziri Ahmed ameliita tukio hilo kuwa ni jaribio la mapinduzi, Huku akikemea watu wenye nia ovu ya kuigawa Ethiopia kuacha mara moja.

Mji wa Ahmara umekuwa ukikubwa na machafuko mara kwa mara, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ukabila na masuala ya kisiasa.

Tayari Ubalozi wa Marekani nchini humo, umetoa tahadhari kwa wananchi wake wanaoishi mjini Addis Ababa kuishi kwa tahadhari kufuatia tukio hilo.