Mkurugenzi wa Shirika la fedha la kimataifa (IMF) Bibi Christine Lagarde amesema mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na China hautakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa yoyote.

Akiongea na waandishi wa habari nchini Malaysia, Bibi Lagarde amesema mazingira ya mvutano wa biashara sio mazuri kwa biashara ya dunia. Amesema nchi zilizojiunga na mnyororo wa uzalishaji kama Malaysia, uchumi wake unaweza kudidimia.

 Amesema IMF ilikadiria kuwa uchumi wa nchi hiyo utakua kwa asilimia 4.5, lakini kutokana na mvutano wa kibiashara makadirio yaliyotolewa na serikali ya nchi hiyo ni ya chini. Ameongeza kuwa IMF ina wasiwasi kuwa mvutano wa kibiashara utakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa dunia, na wanatarajia kuwa kabla ya kufikia mwaka 2020 uchumi utapungua kwa asilimia 0.5.