Mtangazaji Maimartha Jesse amedai kuwa hamchukii mzazi mwenzake na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zarinah Hassan ‘Zari’ kama watu wanavyodhani bali ni kazi yake kama mpashaji habari ndiyo inamfanya ‘amchane’.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Maimartha alisema yeye siyo Team Mobeto ila kazi yake ndio sababu ya yeye kumsema Zari pale anapokuwa amekosea lakini hakuna sababu yoyote na hamchukii kama watu wanavyomchukulia. “Watu wanahisi mimi namchukia Zari lakini hakuna ukweli wowote, Zari nampenda sana na ni mwanamke ambaye ana ushawishi ila pale anapokosea namkosoa kama mtu mwingine anavyoweza kukosolewa, mimi wala si Timu Hamisa,” alisema Maimartha.