Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha ameweka wazi kuwa yupo Single kwa miaka mitano sasa na hajawahi kukutana na mwanamke tangu alipoachana na mke wake Flora Mbasha.Mbasha amefunguka hilo kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Ijumaa Juni 21, 2019 akijibu swali la Sam Misago juu ya ukaribu wake na mtoto wake wa kike Elizabeth huku akiwa hana mwanamke.

''Toka April 2014 nimejitunza sijawahi kukutana na mwanamke kimwili, mimi ni mwanaume niliyekamilika kuanzia mwonekano lakini kwasasa sina mwanamke namjali tu mtoto wangu ili ajivunie uwepo wa baba yake ila Mungu akijaalia nitapata mke'', alisema.

Kuhusu skendo zinazoendelea mitandaoni kuwa mwimbaji huyo ana watoto wengi tu na sio mmoja kama anavyodai yeye, Mbasha aliweka wazi ukweli.

''Nina mtoto mmoja tu ambaye ni Elizabeth Mbasha, ila hao wanaosema nina watoto wengi ni uzushi tu wa mitandaoni pia ni uongo na wivu wenye lengo la kunichafua lakini watashindwa kwa jina la Yesu''.