Pamoja na kuwa hana historia ya kucheza soka England wala hajawahi kuishi katika taifa hilo, Diego Maradona ameamua kuweka wazi hisia zake juu ya kuitamani ajira ya kocha wa sasa wa Man United Ole Gunnar Solskjaer na anaamini anaweza kuwa mbadala sahihi katika kiti hicho.

Maradona ambaye hana CV nzuri katika nafasi ya ukocha tofauti na kiwango chake enzi anacheza, ameeleza kuwa Man United ndio club pekee ya England ambayo amewahi kuiota kuifanyika kazi na anaomba kama watakuwa wanafikiria kutafuta kocha mwingine ni vyema wamfikirie yeye.

“Kama (United) wanahitaji kocha nafikiri mimi ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo, Man United imekuwa ni club ya England ninayoipenda kwa muda mrefu sana lakini kwa sasa naweza kusema pia Man City, najua ni ngumu kubadili ila ni kwa sababu ya Aguero tunaongea sana na anacheza vizuri pale”>>> Diego Maradona

Historia ya Maradona katika nafasi ya ukocha haivutii sana licha ya baadhi ya vilabu kumuamini na kmpa nafasi, hadi sasa Maradona CV yake inaonesha amekaa katika vilabu kwa muda mchache hadumu sana, kwa sasa akiwa na club ya  Dorados anahangahika kwa msimu wa pili kuipandisha Ligi Kuu timu ya ambayo inashiriki Ligi daraja la pili nchini Mexico kwa sasa.