Mama mmoja wa watoto watano waliouawa na baba yao amelitaka jopo linalosikiza kesi ya mumewe kutomwekea hukumu ya kifo.

Amber Kyzer aliambia mahakama moja huko Carolina ya kusini kwamba Tim Jones Jr hakuwaonea huruma wanangu kwa njia yoyote ile lakini wanangu walimpenda sana.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 37 alihukumiwa mwezi Mei kwa kuwauawa watoto wake wenye umri kati ya mmoja hadi nane nyumbani kwake karibu na Lexington mnamo tarehe 29 Agosti 2014.


Jopo hilo linajadiliana iwapo Jones anafaa kupewa kifungo cha maisha ama kunyongwa. ''Nasikia kile ambacho watoto wangu walipitia'', alisema bi Kyzer katika mahakama siku ya Jumanne.

''Na kama mama iwapo ningekuwa na uwezo wa kuupasua uso wake ningeupasua. Hicho ndio nilicho nacho ndani yangu''.


Timothy Ray Jones akionekana katika mahakama ya Lexington tarehe 4 mwezi Juni
Bi Kyzer aliambia jopo hilo kwamba alikuwa akipinga hukumu ya kifo kwa kipindi chote cha miasha yake

Alisema kwamba licha ya kutamani sheria 'imkarange' mumewe asingepenedelea kumchangulia hukumu ya kifo.

''Hakuwaonyesha watoto wangu huruma yoyote'' , alisema. ''Lakini watoto wangu walimpenda na iwapo ninazungumza kwa niaba ya yangu na watoto wangu basi hilo ndio tamko langu''.

Bi Kyzer hatahivyo alisema kwamba ataheshimu chochote kitakachotolewa na jopo hilo la majaji.

Alikuwa ameitwa kutoa ushahidi wake na mawakili wa mumewe.

Wanandoa hao walifunga ndoa wiki sita baada ya kukutana 2004 wakati wote walipokuwa wakifanya kazi katika bustani ya watoto ya kucheza katika eneo la Chicago