Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ameinunua Jezi ya Timu ya Taifa Stars kwa Tsh. Milioni Tano.

Bi Samia ametoa fedha hizo kama mchango wa hafla ya harambee  kuichangia Taifa Stars inayofanyika leo katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

“Mimi nitanunua fulana ya Taifa Stars kwa shilingi milioni tano,” Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  tayari kiko Misri kwaajili ya mashindano ya Africa, AFCON 2019 ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi hapo kesho. Tayari Spika wa Bunge, Job Ndugai amewasili nchini humo kwaajili ya kuipa hamasa Timu hiyo