Jina la Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya limeendelea kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii, hiyo inakuja ni kutokana na taarifa zilizokuwa zimetolewa awali kuwa mwanariadha huyo kabla ya kushiriki mashindano ya riadha atapunguzwa homi.

Caster Semenya mwenye umri wa miaka 28 aliripotiwa kuwa na homoni za kiume kwa wingi kuliko za jinsia yake ya kike, hivyo baadhi ya watu walitaka kuwa apunguzwe homoni hizo ndio aendelee kushiriki mbio za riadha za wanawake, Caster Semenya ni mshindi wa medali mbili za dhahabu alizopata katika michuano ya Olympic.

Baada ya Mahakama ya michezo CAS kutangaza kuwa mwanadada huyo apunguzwe homoni za kike, Caster Semenya mwenyewe aliamua kukata rufaa na kuipelekea kesi hiyo nchini Uswiss ambapo leo limetoka zuio kwa muda kuwa walau hadi June 25 ndio wasikilize tena, shirikisho la riadha duniani IAAF linalazimika kuheshimu amri ya Mahakama