Lulu Diva alinipa laki tano tufanye kiki - TID
Msanii wa Muziki, TID amesema kuwa Lulu Diva alimtuma mtu ampe laki tano ili amzungumzie apate kiki.

TID amesema kuwa maisha yake ni kiki, huku akisema kuwa hata wale wanaohitaji Kiki anawatoza fedha na anafanya kiki.

"Hivi unajua kuna watu wanatafuta kiki kupitia mimi na kunipatia pesa, huwezi amini Lulu Diva ameniletea pesa ili nimzungumzie apate kiki," TID ameiambia Wasafi Tv.

"Kamtuma mtu kamwambia mwambie TID anitafutie kiki shika laki tano , tena watu wengine wakitaka kiki nawacharge , lakini mimi maisha yangu ni Kiki automatically."