Mkali wa midundo ya Bongofleva kwa muda mrefu Lamar, kutoka Fish Crub Records, ametangaza rasmi kurejea mzigoni baada ya kuacha kazi hiyo kwa miaka kadhaa.

Lamar amesema kurejea kwake kutasaidia muziki wa Bongofleva kupiga hatua zaidi kwani kuna kitu chake cha tofauti anaamini kinakosekana kwasasa.

Kwa upande mwingine, Lamar amesema zipo kazi nyingi ambazo zipo Library alifanya na msanii mkongwe Chid Benz hivyo atazifanyia kazi na zitamrejesha mkali huyo wa michano.