Mwimbaji, muigizaji na mjasiriamali Shilole ameamua kuuliza swali leo kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa ni kwanini wasanii hasa wa kike hupenda kudanganya kuhusu umri wao? ishu hii imeonekana kuwakera wengi mtaani kuhusiana na wasanii wengi kujishusha umri.

Siku kadhaa zilizopita ishu hii ilimkumba mwimbaji Gigy Money ambapo mpaka ilifikia hatua ya kuonyesha cheti chake cha kuzaliwa ili kuwathibitishia wadau kuwa ana miaka 22 kutokana na madai ya wengi kuhisi kuwa anadanganya umri wake na hafananii kuwa na miaka 22.

“Ivi kwanini wasanii haswa wakike wanapenda kudanganya umri wao ?????? 😂😂 kiukweli mimi mwezi wa 12 natimiza 31” aliandika Shilole“Mkitaka Na Passport ntawapostia Na mama angu ntawapa mumfamyie Interview 🤣” aliandika Gigy Money