BAADA ya kuzaa watoto wawili kabla ya kuolewa huku kila mtoto akiwa na baba yake, mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto amefunguka kwamba kwa sasa hafikirii tena kufanya hivyo.



Akipiga stori mbili-tatu na gazeti hili, mrembo huyo alisema kuwa katika maisha yake hakuwahi kuamini katika ndoa ndiyo maana akaamua kuzaa watoto wawili bila ndoa, lakini sasa anatamani kuongeza watoto wengine watano ndani ya ndoa ili atimize ndoto yake ya kuwa na watoto saba.



“Sasa hivi ninahitaji mwanaume wa kufunga naye ndoa na Mungu akitujalia nizae naye watoto watano ili nitimize ndoto yangu ya kuwa na watoto saba,” alisema Mobeto. Katika watoto wawili alionao Mobeto, mmoja amezaa na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mwingine amezaa na Mkurugenzi wa EFM na TVE, Francis Ciza‘Majizo