Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata viongozi watatu wa Baraza vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) akiwepo Petric Sosopi (Mwenyekiti BAVICHA) wakiwa mji mdogo wa Ifakara wilayani Kilombero wakituhumiwa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.

Wengine waliokamatwa ni Daniel Ngogo na mwingine hajafahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,  Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao wamekamatwa Ifaraka na wapo njiani kupelekwa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro.

"Watakapofika tutawafanyia mahojiano, walikuwa wakifanya kampeni za nyumba kwa nyumba wakati wakijua ni kinyume na kipindi cha kampeni hakijafika," amesema Mutafungwa.