Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alionekana akitetemeka kwa mara nyingine tena mjini Berlin Alhamisi wakati wa hafla mjini Berlin , siku nane baada ya kufanya hivyo

Video inayoonyesha Bi Merkel, 64, akijikunyata kwa mikono yake huku mwili wake ukitetemeka badaa ya dakika kama mbili alionekana kurejea katika hali ya kawaida na akasalimiana kwa mikono na waziri mpya wa sheria wa Ujerumani.

Alipewa glasi ya maiji ya kunywa, lakini hakuyanywa.

Katika tukio la awali Bi Merkel alisema kutetemeka kwa mwili kulitokana na upungufu wa maji mwilini.

Baadae aliondoka kuelekea katika mkutano wa G20 mjini Japan mchana kama ilivyokuwa imepangwa.

Jinsi Kenya ilivyoizamisha Tanzania
Je Marekani ina malengo gani Iran?
Wachimba mgodi 36 wafariki DR Congo
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 28.06.2019
" Mambo yote yanaendelea kama ilivyopangwa. Kansela wa shirikisho yuko salama," alisema msemaji wake Steffen Seibert.

Shirika la habari la Ujerumani DPA lilisema kuwa licha ya kipindi cha joto nchini humo , joto lilikuwa limepunguwa wakati wa hafla iliyofanyika katika kasri la Bellevue , ambako rais Frank-Walter Steinmeier alikuwa akimtangaza waziri mpya wa sheria Christine Lambrecht.

Mara ya mwisho , Bi Merkel alitetemeka alipokuwa amesima kando ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky chini ya jua . Alisema alijihisi vizuri baada ya kunywa maji.

Siku ya Alhamis alihudhuria kuapishwa kwa Bi Lambrecht bungeni (Bundestag)kwa muda mfupi -na baadae akaondoka.

Atakaporejea kutoka Japan, Bi Merkel atakabiliwa na mazungumzo magumu mjini Brussels wakati ambapo yeye na viongozi wengine wa Muungano wa Ulaya kumtafuta mgombea wao urais wa tume ya Muungano wa Ulaya atakayechukua nafasi ya Jean-Claude Juncker.

Anaweza kuwa na tatizo gani?

Duru za serikali zimeviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kuwa hakukuwa na cha kuhofia na alipokuwa anaondoka kuelekea Osaka, msemaji wake alituma ujumbe wa tweeter kwamba" mazungumzo ya ushirikiano yamepangwa na wakuu wengine wa serikali na nchi".

Hata hivyo, Bi Merkel alikuwa na tatizo la kutetemeka wakati wa hali ya hewa ya joto alipokuwa katika zira nchini Mexico in 2017, alipokuwa akihudhuria sherehe za kijeshi.

Alifanyiwa uchunguzi mwingi wa kimatibabu na hakuna tatizo lililopatikana, kulingana na taarifa. Hakuna ushahidi , kwa mfano wa ugonjwa wa mishipa wa Parkinson ,ambao humfanya mtu kuwa na dalili za kutetemeka kwa mwili.