Mjasiriamali Chum Makame Chum akielezea changamoto wanazokutana nazo katika utendaji wa shughuli zao kwa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati hiyo kukagua shughuli wanazozifanya visiwani Zanzibar. 
 Machano Haji akitoa maoni yake kwa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA iliyopo Zanzibar inayoendelea na ziara yake ya kukagua Wajasiriamali waliowapatia mafunzo visiwani Zanzibar. Wajasiriamali hao waliiomba Kamati hiyo kusaidia kupata Soko la bidhaa wanazozozalisha.

 Mratibu na Katibu wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Tanzania Dkt. Seraphia Mgembe akizungumza na Wajasiriamali wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja ambapo Kamati hiyo ipo visiwani Zanzibar kukagua shughuli zinazofanywa na MKURABITA Zanzibar.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA wakikagua bidhaa kutoka kwa Mjasiriamali Asha Juma huko Kinduni Kaskazini Unguja. Kamati hiyo ilietembelea Wajasiriamali wa Kaskazini na kusikiliza maoni yao ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati hiyo kukagua shughuli wanazozifanya visiwani Zanzibar. 
Mfanyabiashara wa Mchele Visiwani Zanzibar (Zanzibar Rice)Yussuf Faki akitoa maelezo kwa baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati hiyo kukagua shughuli wanazozifanya visiwani Zanzibar. Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar