Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Uganda Jose Chameleone hapo jana ameamua kufuata nyayo za Bobi Wine kwa kuingia kwenye siasa.



Inaelekea umekuwa ni mtindo wa kawaida kwa wanamuziki maarufu kugeuka kuwa wanasiasa. Bobi Wine amekuwa akizingirwa na utata wa kisiasa tangu alipogombea kiti cha ubunge mwaka 2017.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Jose Chameleone ambaye jina lake halisi ni Joseph Mayanja amesema kuwa anataka kuwa Meya wa mji mkuu wa Uganda Kampala. Amenukuliwa na gazeti la Uganda Observer akieleza.

Chameleone anakiri kuwa ameshawishiwa na Bobi Wine

Chameleone ni mmoja wa wanamuziki maarufu katika eneo la Afrika Mashariki.

Moja ya nyimbo zake zinazofahamika ni ule wa Shida za Dunia, unaozungumzia matatizo yanayowakabili watu:

Akielezea matarajio yake, amesema:”Wakati huduma zinapokuwa katika hali mbaya, watu wanaanza kuamka .Watu wana kiu ya uongozi unaofaa na hawajaupata”.

“Wale wanaodhani kuwa ni mkumbo wa Bobi Wine wana ukweli kiasi fulani ,” Chameleone alinukuliwa akisema.

Bobi Wine alipiga kengele halafu akasema ‘Tumekuwa watu wazima wa kutosha sasa ; Tunaweza kufanya hili ‘. Kwani kuna shida gani ya kufanya hilo? Kila kitu katika dunia hii kina mtu fulani aliyekianzisha .”

Chameleone anakiri kuwa ameshawishiwa na Bobi Wine. Muimbaji huyo wa kibao ”Badilisha” anaaminiwa kuwa amekuwa mfuasi wa chama tawala cha NRM, ambapo amekuwa akitumbuiza kwenye matukio ya chama hizo.

Chameleone hakuficha urafiki wake na mbunge wa Kyadondo mashariki Bobi Wine, hususan pale Wine alipojipata katika utata wa kisiasa na kukamatwa na maafisa wa polisi na kuwekwa mahabusu. Alimtembelea mahabusu kumfariji:

Tangu kuchaguliwa kwake amekwishafanya maandamano maarufu na amekuwa akikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini. Anadai kuwa alipigwa na polisi alipokuwa katika mahabusu ya polisi.