Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashitindi (katikati),akiwa pamoja na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoka  Dar es Salaam jana, ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).
 Mwanasheria wa EfG, akizungumza na wafanyabiasha wa Soko Matola
 Ofisa wa EfG, Eva akizungumza na wafanyabiasha wa Soko Matola
 Ofisa Ufuatilia na Tathmini wa EfG, Samora Julius akizungumza na wafanyabiasha wa Soko Matola
 Mwenyekiti wa Soko la Uhindini, Joseph Mwakitalima akizungumza
 Picha ya pamoja Soko la Uhindini
 Mwenyekiti wa Bodi EfG,akisoma taarifa mbele ya Meya wa Jiji la Mbeya
 Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashitindi (katikati),akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoka  Dar es Salaam jana, ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya, Beatha Mtani,akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni kutoka  Dar es Salaam juzi, ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)

Na Dotto Mwaibale, Mbeya

Meya wa Jiji la Mbeya Mchungaji David Mwashitindi amesema wataongeza nguvu ya kuvisaidia vikundi vya wanawake pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali.

Hayo aliyasema jijini humo jana wakati akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni walioandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoka  Dar es Salaam ambao wapo jijini humo kwa ziara ya mafunzo na kuwahamasisha kujiunga na Umoja wa wanawake Sokoni wa Kitaifa.

"Sisi kama jiji tutahakikisha tunaendelea kuwasaidia wanawake wajasiriamali kwa kuwapa mafunzo na mitaji ili kuinua maendeleo yao na Taifa kwa ujumla" alisema Mwashitindi.

Mwashitindi aliwaomba wanawake hao kuwa kwenye vikundi ili iwe rahisi kujulikana na kupata misaada badala ya kuwa mmoja mmoja.

Aliongeza kuwa wakati wote atakuwa ana watuma maofisa maendeleo ya jamii kutembelea vikundi vya wanawake ili kujua changamoto zao na kuzitatua.

Afisa Maendeleo ya Jamii Beatha Mtani aliwaomba wanawake hao kujiunga pamoja  na kuendelea kuitunza amani iliyopo nchini.

Alisema mahali popote palipo na amani  ndipo shughuli za maendeleo zinafanyika hivyo aliwaomba wanawake hao waendelee kuilinda.

Mtani alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kumkomboa mwananchi wa kawaida ili awe na maisha bora badala ya kuwa na bora maisha.