Kufuatia uzushi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na mauaji ya aliyekua Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Lucas Luhambalimo, Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limezungumzia juu ya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea May 30 mwaka huu katika Kijiji cha Munga Tarafa ya Mtimbira Wilayani Malinyi Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo SACP Wilbrod Mutafungwa anatolea ufafanuzi chanzo cha tukio hilo nakueleza kuwa tayari watuhumiwa watatu wako mbaroni kufuatia tukio hilo