Mwanamama wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel amesema kuwa pamoja na kwamba hayupo tena kimapenzi na mzazi mwenzake, Mose Iyobo ‘Moze’ lakini ukweli ni kwamba wako poa tu na wanasalimiana kama kawa. Aunt aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kugombana kwao kwenye masuala ya kimapenzi hakuwezi kuathiri malezi ya mtoto wao, Cookie kwa vile wao ni wazazi na wana haki ya kuzungumza chochote.

Kuna watu wanajua mimi na Iyobo hata tukionana hatusalimiani, siyo kweli, Yule ni baba wa mtoto wangu hivyo tunazungumza na tunacheka panapostahili,” alisema Aunt ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na Iyobo aitwaye Cookie.