Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Asia Ahmed (52) mkazi wa Kihonda kwa kosa la kumchoma moto mjukuu wake wa miaka 5 kwa kutumia upawa katika sehemu za siri.


Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi bibi huyo amefikia maamuzi ya kumchoma moto huyo kwa madai kuwa amekuwa akikojoa kitandani mara kwa mara.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la Kamanda wa Polisi Morogoro Wilbroad Mtafungwa amesema mtoto huyo pia ni mwanafunzi wa chekechea kupitia tukio hilo limesababishia maumivu makali.

Katika tukio lingine Kamanda mtafungwa amesema Kamanda Mtafungwa wanawashikilia watuhumiwa watano wilayani Kilosa kwa tuhuma ya kuiba vifaa vyenye thamani ya millioni 36, mali ya Kampuni ya YARP MERKEZ ambayo inausika na ujenzi wa reli ya Kisasa ya Mwendokasi.