Komedianii matata Bongo ambaye ni mshindi wa Shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan amewafungukia baadhi ya watu wanaowaposti wenzao kwenye mitandao ya kijamii wakiwa kwenye matatizo au furaha akiwataka kuacha unafiki.



Akizungumza na Gazeti la ijumaa Wikienda, idris alisema kinachomuumiza, hivi sasa watu wengi wamejisahau kuwa kuna umuhimu wa kumfariji mtu uso kwa uso bila mitandao ya kijamii.



“Watu wamekuwa wa ajabu sana, yaani mtu akishamposti mtu kwenye mitandao ya kijamii akiwa amepata msiba au ana jambo lolote, anakuwa amemaliza, lakini ukweli ni kwamba wanapoteza ile hali ya ubinadamu siku hadi siku kwa kuamini akishamposti mtu amemaliza,” alisema Idris.



Aliendelea kueleza kuwa, kwa upande wake yeye anaona ni unafiki kumposti mtu kwenye mitandao bila kumuona uso kwa uso ukiamini kabisa mitandao imemaliza kazi.