Mtoto mdogo wa chini ya miaka mitano alipatikana akilia kwa hofu ndani ya nyumba akisema, "Sitaki kufa ".

Wazazi wake waolikua wameshawishiwa kuwa chanjo ya polio ni salama walijaribu kummtoa nje ashuhudie ndugu zake wakiwekewa matone ya chanjo hiyo mdomoni.

Lakini mtoto huyo aliendelea kulia kwa uwoga. Wahudumu wa afya ya jamii wanaotoa chanjo hiyo walikua wamekatazwa kuendesha kampeini hiyo katika moja ya vijiji nchini Pakistan hadi waliposaidiwa na Dr Uzma Hayat Khan, mshauri wa afya ya umma.

Khan, ambaye ni mshirikishi wa kampeini ya chanjo ya polio nchini anauzoefu wa kuwzungumza na watu wanaokataa watoto wao wapewe chanjo hiyo.

Lakini alikuwa na hofu alipofika katika boma hilo kwa sababu alikutana na kundi la wanaume ambao walimkataza ingie nadi ya nyumba.

Purukushani hilo lilimalizika baada ya jamaa mwingine wa familia hiyo ambaye ni daktari kutokea na kuwasaidia.

Jinsi chanjo zinavyookoa maisha yako
Wahudumu wa afya walifanikiwa kwapatia chanjo watoto wote katika boma hilo isipokua yule aliyekuwa akilia kwa uwoga.

Watu wengi nchini Pakistan wanahofia sana kupewa chanjo ya polio licha ya kuwa inaokoa maisha

Lakini hali ni mbaya zaidi katika mji wa Rawalpindi ambako vurugu zinazotokana na wakaazi ambao hawataki watoto wao wapewe chanjo ya polio ni ni za kiwango cha juu.