Huwezi kuamini!!! Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Harmonize kutoka WCB, amejikuta akimbeba mgongoni mpenzi wake Sarah baada ya kushindwa kupanda Mlima Mkomaindo ulioko mkoani Mtwara.

Tukio limetokea wakati msanii huyo akiwa mjini ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Masasi Rock Festival, lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Wakati wa kupanda mlima huo, Sarah ambaye ni raia wa Italy, alionekana kuchoka na kushindwa kuendelea ambapo katika hali isiyotegemewa na wengi Harmonize ambaye ni mwenyeji wa Mtwara alimbeba mgongoni na kuwaacha watu waliokuwapo hapo kuangua vicheko.

Tamasha hilo linatarajiwa kuisha Juni 9, mwaka huu likiwa na lengo la kutangaza utalii wa ndani ya mkoa wa Mtwara. Kaulimbiu ya Tamasha hilo ni ‘Tukutane Kileleni.’