Jumapili ya June 23,2019 ilikua ni siku kubwa kwa upande wa kiburudani nchini Marekani ambapo ilikua ni siku ya kutangazwa na kutolewa kwa tuzo za BET ambapo Cardi B ameongoza kwa kuondoka na jumla ya tuzo mbili usiku huo.

Katika tuzo hizo kutokea Afrika Burna Boy ameibuka na ushindi katika kipengele cha Best International Act pamoja na Sho Madjozi kutokea Afrika Kusini ambae ameshinda Best New International Act.

Rapper Cardi B aliibuka na tuzo ya Album bora ya mwaka kupitia Album yake ya Invasion of Privacy iliyotoka rasmi April 6,2018 huku Beyonce akitajwa kuchukua tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa RnB/Pop Artist, kundi la Migos likiondoka na tuzo ya kundi bora(Best Group), Marehemu Nipsey Hussle amekumbukwa kwenye kipengele cha Msanii bora wa kiume kwenye Hip Hop.