Mwanamitindo/ Msanii wa Muziki, Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu uhusiano wake na Msemaji wa Simba SC, Haji Manara.

Ikumbwe hivi karibuni kumekuwa na watu wakizungumzia ukaribu wao na kupelekea sintofahamu hali iliyofanya, Hamisa afunguke.

"Mimi na  Haji Manara ni kama mtu na kaka yake, Haji ni kaka angu wa kufikia , ni mtu ambaye naheshimiana nae sana bna hata tukiongea mtu hawezi kufikiria kuna mambo mengine au ukaribu wetu utafsiriwe vibaya hapana mi sipendezewi na hilo," alisema Hamisa.

"Mimi nina watu wengi sana ninao heshimiana nao na wanafamilia zao na mimi sipendi na sifurahishwi nayo kwasababu mimi mwenyewe natarajia kuwa mke wa mtu mtarajiwa."