MWANAMITINDO wa Tanzania Flavianna Matata kuja na bidhaa zake mpya Taulo za kike (pads) kutoka kwenye Kampuni yake ya LavyTaulo ambazo zitaitwa Lavy Sanitary Pads.Kupitia ukurasa wake wa instagram Flavianna aliweka picha ya Bidhaa iyo na kuandika**COMING SOON** ….. Kwanza kabisa tunawashukuru wanawake wote waliokua sehemu ya utafiti wetu katika harakati ya kuhakikisha tunapata pads(taulo za kike)zinazo kidhi mahitaji halisi ya mwanamke.Kwa kupitia maoni ya moja kwa moja ya mtumiaji, tumeboresha na tunaendelea kuboresha bidhaa zetu.
Changamoto ya pads na tampons zenye ubora mzuri kwa bei nafuu bado ni kubwa.Hedhi ni muhimu na fahari ya kila mwanamke hivyo kwanini iwe kero kwa kukosa pads nzuri zinazokidhi mahitaji?
LAVY tunawaletea pads zenye ubora wa hali ya juu kwa bei rafiki.

Pads hizi zitaweza kutumika na mwanamke yeyote anayependa na kuhitaji ‘quality’ ya juu.
Moja kati ya lengo letu kubwa hasa ni kusaidia wasichana mashuleni, hususan wanafunzi wanaotoka kwenye familia za hali ya chini.

Asilimia 10 ya mauzo yetu yote itaelekezwa kwenye miradi ya Maji, Vyoo na Usafi (WASH) mashuleni ili wadogo zetu pia waweze kuwa huru wakati wakiwa kwenye siku zao za hedhi.

Tufurahie uanamke wetu huku tukiwawezesha na kuwainua wanawake wenzetu ambao jambo hili wanalipokea kwa mawazo sana kwa sababu tu hawana nyenzo nzuri ambazo wengi wetu humu pengine ni kitu kidogo sana kwetu.

Endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa zaidi. #lavyproducts