Mwimbaji mkongwe wa Bongofleva Dully Sykes, ameweka wazi kuwa hakuongelea issue ya Fid Q kutumwa soka pale MJ Records miaka nyuma kwa ubaya kwani haya yeye aliwahi kutumwa sana.

Akiongea leo kwenye eNewz ya East Africa Television, mkali huyo amekiri kuwa kama Fid Q anaona amekosea sehemu amsahamehe lakini ukweli ni kwamba wakiwa vijana wadogo walipitia msoto sana wa kutumwa na wakubwa zao.

''Mimi mwenyewe nimetumwa sana soda na nilikuwa naonana naye pale MJ Records kwahiyo kutumwa ilikuwa suala la kwaida na kama amemind naomba anisamehe'', amefunguka Dully.

Kwa upande mwingine Dully amesema dhana iliyopo sasa kuwa bifu za wasanii ndio zinaweza kumpandisha msanii sio kweli na kama ikiwa hivyo basi yeye hahitaji hilo na anatamani kuwa na historia nzuri.