Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwaongoza wapenzi na wanachama wa Klabu ya Yanga kwenye tukio la uchangiaji wa timu hiyo utakaofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba, Juma Nature pia wanatarajiwa kuwa miongoni mwa wasanii 15 watakaotumbuiza kwenye tukio hilo kubwa linalotayarajiwa kuiwezesha Yanga kuendeshwa kisasa.

Akizungumza  jana, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya kuhamasisha uchangishaji , Dk David Ruhago alisema kuwa tukio hilo Kubwa kuliko linatarajiwa kuwakutanisha wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kwa lengo la kuchangisha fedha ambazo zitaisaidia timu hiyo kusajili na kuendesha klabu kisasa.

"Ninawaomba wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwenye tukio hilo ikiwa ni pamoja na kununua tiketi kuweza kuichangia timu hiyo ili waweze kufikia malengo walinayotarajia kuyafikia.

"Dk Kikwete anatarajiwa kutuongoza hivyo mnapaswa kujitokeza siku hiyo,"alisema na kuongeza kuwa mashabiki wamerahisishiwa kununua tiketi na kwamba kwasasa zinapatika kwenye simu.