Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja Abdallah Bushiri Shija (42), mkazi wa Igodima Jijini Mbeya  kwa tuhuma za kufanya kazi za utabibu bila kuwa na taaluma ya utabibu hususani kwa magonjwa ya wanawake wenye matatizo ya uzazi.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa hakuwa na kibali chochote cha kufanya shughuli hiyo wala cheti chenye taaluma hiyo na alikiri kuwatapeli wahanga hao pesa Tsh. 2,472,000 kwa madai kuwa atawasaidia.

Hata hivyo alishindwa kutatua matatizo ya wahanga hao ikiwemo kupata ujauzito. Katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa mtuhumiwa vilipatikana vifaa tiba na dawa za Hospitali za Serikali (MSD) kama ifuatavyo.