STAA wa filamu ambaye hivi sasa amegeukia ufundi cherehani, Jacqueline Wolper, amefunguka kuwa dharau zake zilimfanya asiwe tajiri wa kike (boss lady) kwa kuwapotezea mapedeshee na watu wenye pesa zao.  Akipiga stori na paparazi wetu, Wolper alisema kuna wakati watu walitaka kumtumia ndivyo sivyo kwa sababu ya pesa zao, lakini akawadharau na kuendelea kufanya yaliyo sahihi.

“Unajua kuna vitu nilikuwa navidharau sana, siyo kwamba nilikuwa sitamani kuwa mwanamke mwenye hela bali nilitaka kuishi maisha ya kujitafutia mwenyewe ambapo pale unapokosa unafanya bidii tena ya kusimama lakini sio kumtegemea mtu ndio maana nilikuwa na dharau sana,” alisema Wolper.