Msanii wa muziki, Queen Darleen amesema kuwa Diamond na AliKiba zingekuwa hazivii (hawapatani) nyimbo za msanii huyo zisingepigwa Wasafi Tv, hivyo hakuna kitu kama hicho.

Kuhusu ukaribu wake na AliKiba amedai kuwa ukaribu wake na Msanii Ali Kiba umepungua kutokana na majukumu ya kifamilia aliyonayo.

"Unajua maisha yamebadilika tulikuwa watoto, tulikuwa hatuna familia lakini mwisho wa siku kila mtu kagawanyika na majukumu yake Ali ameowa na yupo na familia yake kwa hiyo kila mtu na maisha yake, majukukumu ndio yanatuweka mbali,"Queen Darleen ameiambia Wasafi Tv.

Queen Darleen na Ali Kiba waliwahi kufanya kazi pamoja nyimbo inayoitwa 'Wajua'.