Msanii wa Bongo Fleva, Christian Bella, ameweka wazi  juu ya fununu kuwa anatoka na msanii, Hamisa Mobetto.

 Bella amesema kuwa "Mimi na Hamisa tunafanya kazi pamoja, tupige story watuombee mazuri, msapoti Hamisa mfanye vizuri, mfanye shoo nini na nini watuombee sio waseme mambo ya sita kwa sita kama yale mambo ya kwichi kwichi hakuna hayo mambo."

 Bella amesema hayo akipiga stori na eNewz ya EATV, ambapo amesema kuwa pindi anapomuona Mobetto anaona sura za watu ambao ameshatoka nao, jambo ambalo linaweza kumfanya aonekane tofauti.

"Shemeji kabisa, ukimuangalia kuna sura za washkaji kabisa, kidogo watauliza 'vipi mzee'", amesema Christian Bella.